Namshukuru Mungu Kwa kutuvusha tena Kwa ushindi mwaka huu.
•Utangulizi
Wakati najiandaa na kumuomba Mungu juu ya Yale ninayotamani kuyafanya Mwaka 2025, Roho mtakatifu alinielekeza pia kuomba ili nifahamu Mungu amekusudia jambo gani kwangu Mwaka huu.
#. Kwanza kabisa, ni vizuri kuwa na mipango lakini ni muhimu kufahamu kwamba Mungu anayo mipango yake pia kulingana na majira ya maisha Yako.
Naona una malengo yako lakini Je! unayafahamu malengo ya Mungu juu Yako?
Utayafahamuje? nenda kwenye kikao barazani pa Bwana. Tenga muda mchache wa muhimu wa kuyaombea hayo uliyopanga na atakuambia lipo litafanyika na lipi lianze Tena Kwa namna gani lianze. Kina nani ushirikiane nao n.k na kama asipo kupambia Kwa sauti ataruhusu ufahamu uhalisia wa watu unaoshirikiana nao ili aweke umakini ndani yako wa namna ya kufanya nao kazi.
Anaweza pia kuruhusu usome kitabu muhimu au uhudhurie semina itakayo fungua mawazo na ufahamu wako juu ya Hilo jambo.
Mambo Muhimu
1. Mahusiano na Mungu.
Unafanya kazi kubwa sana kuzitafuta nguvu za Mungu kuliko kazi ya kuzilinda.
Hii ni hatari kwako kwasababu ni sawa na mtu anayetafuta Mali Kwa gharama kubwa alafu anazitunza kwenye nyumba isiyo fungwa milango. Utapoteza muda mwingi, bila matokeo unayoyataka. Kuna mambo yatahitaji mahusiano yako na Mungu kuwa mazuri ili yatokee bila kutumia nguvu kubwa.
Yakobo 4:8 (Kumkaribia Mungu naye kutukaribia)
Kama utalinda kile unachopokea kwenye ibada ya katikati ya wiki au ibada ya jumapili basi kufunga na kuomba kitakua ni Kwa ajili ya Yale mengine yasiyowezekana isipokuwa Kwa kufunga na kuomba.
Ameniambia hakuna maana ya kukesha kumwomba Mungu alafu huwezi kukesha kulinda ulimi wako, kulinda moyo wako, kulinda mawazo Yako, macho Yako n.k
Lazima uelewe kwamba nguvu za Mungu unazopokea ni za thamani sana usizipoteze kihivi hivi tuu.
2. Matumizi ya muda
Muda wako wa thamani unautumiaje?
Mfano mrahisi, simu yako vs bibilia Yako. Najua simu ina bibilia pia. Na simu ina vitabu. Ila pia simu ina TikTok, fb, insta, na hata huko unaweza pata mambo ya kuongeza thamani. Suala kubwa ni kuwa makini na matumizi ya muda wako na juu ya kufahamu je hili ninalolifanya hapa linaniongezea thamani au linaniongezea changamoto?
Kama Mwaka huu utatumia muda mwingi kwenye mambo yasiyo kuongezea thamani basi jiandae kupunguza kiwango cha ufaulu wa mipango yako.
Badala ya kujua nani amefanya Nini, unaweza kujikita kujifunza mambo mapya au kuongeza ujuzi kwenye Yale unayoyafanya kupitia hiyo hiyo simu yako.
Sina ugomvi na simu ila, nakukumbusha uwe (specific) na kile unachokifanya kwenye simu yako.
Kina matokeo gani kwako? Ukikuta matokeo hayakufai achana nacho.
Nitaendelea.
3. Mahusiano na Watu.
Ni wazi kwamba watu ndio huinua watu wengine, lakini pia Watu ndio wanaoweza kukushusha. Napenda kurejea baadhi ya maneno ya kiongozi wetu mkuu katika nchi Mhe. Samia Suluhu Hassan, "Watu ni mashahidi wa Mungu".
Mwaka huu jitahidi sana kuwa na mahusiano rafiki kwa ajili ya hatma yako. Utafanikiwaje?
Kwanza yale unayopenda kufanyiwa, wafanyie wengine. Usipoteze muda na watu ambao hawaongezi thamani katika maisha yako. Sijasema uwadharau, hapana!! Sijasema uwapuuzie, hapana ila linda sana matokeo wanayoweza kuya leta kwako mnapokuwa pamoja nao.
Tafuta ukaribu na watu wenye ndogo kubwa, watu wenye maono makubwa, bila kuwadharau hawa wadogo.
Mwaka huu mtu asiye na matokeo asikushauri! Unaweza kusikiliza hekima zake ila usiziweke moyoni mana mara nyingi kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake.
Katika kuhusiana na watu, tengeneza thamani yako, watu sahihi watavutika kwako. Ni vizuri kutumia nguvu kuwatafuta watu wapya lakini ni vizuri zaidi kuboresha vile ulivyo mana watu wa thamani watakutafuta tu!.
Unaboreshaje? Unavaaje kama mtu mwenye safari ya ukuu au kama watu wa kawaida? Unazungumzaje? Unashiriki kwa namna gani kwenye mambo ya wengine, vipi matumizi yako ya fedha(tuytaizungumzia zaidi hii pia), ushiriki wako kwenye jamii iliyopo karibu nawewe je?
Mtu akikusikiliza Kwa dakika kumi anaweza kufahamu ni mtu wa namna gani. Kichwani kwako umeweka vitu gani? Njia ya mwanzo ya kujiongezea thamani ni kuongeza ufahamu wako.
Tafuta eneo moja ambalo unalipenda au unalifanyia kazi alafu ujikite kuongeza ufahamu katika hilo eneo, japo sio lazima liwe eneo lako la kiutaalamu.
4. Nidhamu ya fedha.
Unapenda kutumia kiwango ambacho hakiendani na kiasi unachoingiza.
Nidhamu ya fedha inaendana na ufahamu sahihi wa elimu ya umiliki wa fedha ambayo mara nyingi haifundishwi shuleni.
Unaweza kujifunza Kwa watu waliofanikiwa au kupitia vitabu vingi ambavyo vimeeleza juu ya nidhamu ya fedha au namna ya kuimiliki.
Kwa kifupi tu mwaka huu kama hujaorodhesha mipango yako bado, unahutaji kukaa na kufanya hiyo kazi. Na mpango wa kwanza uwe kuweka akiba ya angalau matumizi yako ya miezi mitatu.
Maana yake hapo uweke kiasi Cha pesa ambacho utakua na uhakika wa kuendelea kuishi Kwa miezi mitatu mfululizo hata usipo pata ingizo lolote jipya la kipato Kwa muda huo.
Hii inakupeleka moja kwa moja kwenye bajeti. Unaijua bajeti yako ya mwezi? Hii inakulazimisha utafute kufahamu ratiba ya matumizi, chakula, safari n.k
Tabia ya kutumia kwasababu vipo, au kupooza moyo kama wanavyodai wengine imesababisha watu wakachukulia poa fursa walizokutana nazo ambazo zingebadilisha maisha yao.
Hii ndiyo sababu unaweza kumkuta mtu asiye na kipato maalum akifanya maendeleo wakati mwenye kazi na kipato maalum akiwa hajafanya chochote.
Mfano mdogo.
Ukinunua simu ya milioni moja wakati unauwezo wa kununua ya milioni tatu, huo ni ufahamu wa kiuchumi.
Lakini..
Ukinunua simu ya milioni moja wakati uwezo wako ni wa kununua ya milioni moja, hilo ni kosa la kiuchumi.
Haya sio maneno mageni mjini, labda Kwa mgeni mjini. Mwaka huu tujifunze sana namna ya kumudu fursa zinazopita mikononi mwetu, ili tusije kufika mwisho na majuto ya kutokufanya vizuri.
Nitaendelea. .