Monday, July 22, 2019

UAMINIFU

                         UAMINIFU.
BWANA YESU ASIFIWE!!
Na Mwl....
.....Karibu katika somo letu la uaminifu.....

Mwisho wa somo hili utaweza kujijibu maswali haya na mengine mengi.

Uaminifu ni nini?
Mimi ni mwaminifu?
Je ninahitaji kuwa mwaminifu?
Inawezekana nikakosa uaminifu?
Je nahitaji uaminifu katika mambo gani?

Tuanze kuangalia haya.
Soma Mathayo 25:14 ..
Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
And unto one he gave five talents, to another two, and to another one; to every man according to his several ability; and straightway took his journey.

Ni wapi/kivipi tunapaswa kuwa waaminifu?
(A) Kuwa waaminifu mbele za Mungu,
  1Korintho 1:9
  1Korintho 4: 1-2
   Torati 7:9
Mungu Mwenyewe ni mwaminifu na yeye ni chanzo cha uaminifu

(B) Kuwa waaminifu kwa watu wengine.
Mathayo 24:45-47 Kuna kuiniliwa baada ya uaminifu,
Kama wewe sio mwaminifu unaiabisha imani uliyonayo wewe. Lakini pia uaminifu unathaminisha wokovu ulionao.

(C) Kuwa mwaminifu katika vyote ulivyo navyo(Mali na mapato yako)
Haswaa! hapa imetupasa kuwa waaminifu katika suala moja msingi kabisa ZAKA na sadaka..
Usiwemwizi wa zaka uwe makini usikose mbingu..

MUNGU ANATUPIMA UAMINIFU KWA YAPI?

- Nafasi tunayompa katika maisha yetu ya kawaida, tunamtambua Mungu kama nani?

- Pesa umeipa nafasi ya ngapi... Siku za mwisho watu watapenda pesa kuliko kumpenda Mungu. Wapo wanaochukiana kisa pesa..

-Biashara au shughuli inayokuingizia mapato, wengi wamekamatwa hapa, maana unaweza ukategwa kwa wateja kuongezeka muda wa ibada.

-Nadhiri na maagano.
Muhubiri 5:4 Ukimwekea Mungu nadhiri usikawie kuiondoa, Mungu hawi radhi na wapumbavu.
  Ni afadhali usiweke kabisa kuliko kuiweka na kutoitimiza.
-Muda wako kwa Mungu, je unampa Mungu nafasi, kuanzia wewe binafsi?. Unashiriki maombi na taratibu zote za ibada?   !!!!!Jitathmini!!!!
Luka 16:10
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
He that is faithful in that which is least is faithful also in much: and he that is unjust in the least is unjust also in much.
Bila kuwa waaminifu haswa kwa mambo madogo kabisa hatuta mwona Mungu,
Nakazia tena sisi ni mabalozi wa Kristo hivyo imetupasa kuwa waaminifu sana mbele za Mungu na mbele za wanadamu.

Haijalishi ni tatizo ama uhitaji wa namna gani, sema kweli hata kama itakugharimu kwa sababu Uaminifu ni pamoja na ukweli.....
 
Usipende usingizi usije ukawa masikini, usingizi si hatar kwa maendeleo tu ya kiuchumi Bali hata kiroho, usiusikilize mwili ukaacha kuyatenda mapenzi ya Mungu..

Ukubwa au udogo wa jambo usikuchanganye!! Uaminifu ni katika mambo yote.

Mungu akubariki sana. Nakutakia wakati mwema.

Mwl. Faraja Komba

Monday, July 8, 2019

Hakuna mahusiano Bila Mawasiliano.

Na .Mwl Wetu..
Bwana Yesu asifiwe.
Developing Devotional relationship with God
Kuna aina saba za mahusiano
1: Wewe na Mungu
2: Wewe na mpenzi au mtu wa karibu sana mfano mke, mume au mchumba
3:Wewe na familia yako (mjomba n.k)
4: Familia hii na familia nyingine
5:Wewe  na Kanisa
6: Wewe na ufalme( wana wa Mungu ambao sio washirika wenzako katika kanisa moja)
7:Wewe na ulimwengu/dunia

Leo tutaangalia zaidi mahusiano kati yako na Mungu., haya yamebeba  msingi wa kila aina ya mahusiano unayopaswa kuwa nayo.

1. Uhusiano kati yako na Mungu  unaoneshwa na namna gani unamjua Mungu na kumpenda Mungu, Na kumjua Mungu nikulijua neno lake na kulitenda

Huwezi kusema unamahusiano na Mungu wakati huna mawasiliano naye.,Huenda mawasilano yenu yameingiliwa na jambo lingine..
   We have much time to pray but no time to listen from God.
Huwezi kuwasiliana na Mungu wakati wa uhitaji tu na ukasema unamahusiano mazuri na Mungu.
Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni lolote ..
 
Listening .. Unauwezo wa kumsikiliza Mungu?
Je unasoma neno lake??
Develop a Conversation with God

Relational prayer, kuna wakati unapaswa kwenda Mbele za Mungu kuimarisha uhusiano wako na Mungu na sio kwenda mbele zake kila saa for your needs/probpems

Reference
Mwanzo 3:24
Dhambi inadhoofisha uhusiano wako na Mungu.
Yohana 17:3
Mwanzo 3:8
 
Watu wengi wa Leo wanamuda mwingi wa social network kuliko muda wao na Mungu, hawawezi au wamesahau kutafuta relationship na watu kuliko Mungu.
Vijana wanatafuta wenzi wao kwa juhudi kubwa kuliko kumtafuta Mungu na kuimarisha uhusiano wao na Mungu.
  Make a room for God in your heart
...
Mungu akubariki tutaendelea wakati mwingine kwa neema ya Kristo. Nakusihi sana imarisha uhusiano wako na Mungu.
*Spend more time with God!!

Barrier/kikwazo kikubwa katika mawasiliano yetu na Mungu ni dhambi na uovu, 
Tukaze mwendo watumishi wa Mungu..
.... To be continued......

Mahali Casfeta Tayomi Mwecau. Monday Service.

WATU WANGU WAJIBU WANGU. MY PEOPLE MY RESPONSIBILITY

 ✓ WATU WANGU WAJIBU WANGU ✓My people my responsibility *NI MUHIMU KUFAHAMU KWAMBA UNATAWAJIBIKA KWA WATU WAKO KATIKA MAMBO YOTE. YAANI YAKI...