Saturday, September 6, 2025

GHARAMA YA USHINDI

 GHARAMA YA USHINDI

1. Utangulizi

2. Gharama ya ushindi

3. Kudumu kuwa mshindi


Sehemu ya kwanza. Utangulizi 

Kila jambo unalo ona limekwisha fanyika, linafanyika sasa au imepangwa kufanyika baada ya wakati fulani, katika mpango wake Kuna kipengele cha gharama.

Gharama ya jambo inaweza kwa sehemu kubwa kuamua thamani ya Hilo jambo hilo ikishirikiana na matokeo yake. 

Tutajikita zaidi kuangalia gharama ya ushindi katika mambo yamuhusuyo mwanadamu hapa duniani. (Maisha) 

Kwa sababu maisha ni jambo pana lenye tafsiri nyingi nitajitahidi kueleza bila kutumia misamiati migumu na Kwa lugha inayoeleweka. Twende pamoja. . .

Gharama ni aidha muda, nguvu, fedha, mali, maumivu, ufahamu/ujuzi, aina ya maisha, aina ya kazi na mambo yanayofanana na hayo yanayofanyika ili kufanikisha jambo lililokusudiwa Kwa muda mfupi au muda mrefu. 

Mfano wapo watu waliolazimika kuishi maisha ya chini ili wahakikishe wanakamilisha ujenzi, wapo waliolazimika kuongeza ujuzi au kisomo ili wapate aina fulani ya kazi.

Zote hizo ni gharama za ushindi wa Yale waliyo yakusudia. 

Wakati unapanga kufanya jambo au kama hukupanga na umejikuta upo ndani ya jambo, jiulize swali la hili, "ni zipi gharama za jambo hili kufanikiwa?"

Unapozifahamu gharama ni rahisi kuishi kulingana na matakwa ya mafanikio ya jambo lako. 

Wakati mwingine kuzifahamu kunaweza kuhusishwa na woga au hofu juu ya jambo husika, lakini Bado ni muhimu sana kufahamu gharama za kushinda. 

Unapo ona biashara ya mtu inaenda vizuri ujue kabisa kuna gharama ya kusababisha iende hivyo. Unapo ona ndoa ya mtu inaenda vizuri ujue Kuna gharama! Unapo ona maisha ya mtu kidogo yanaenda sawa ujue kuna gharama. 

Kwa lugha nyingine rahisi ki tekinolojia, Kila mara tunachaji vifaa vyetu vya mawasiliano ili kuhakikisha tunaweza aidha kupatikana au kuwapata tunaowatafuta. 

Vivyohivyo tunaweka salio kwenye vifaa hivyo ili tuweze kuwa hewani. Maana yake tumeingia gharama ya kuhakikisha yaliokusudiwa yanafanikiwa. 

Zoezi

1. Andika mambo matatu unayojishughulisha nayo katika maisha yako.

2. Ainisha gharama ya mambo hayo. 


Sehemu ya pili. Gharama ya ushindi 

Kwa kiasi sasa tumeshatambua tunacho kumbushana. 

Zifuatazo ni gharama ambazo zinahusika katika kufanikisha ushindi wa mtu au watu katika jambo lililokusudiwa. 

1. Uhusiano na Mungu. 

Huu ni msingi mkuu wa ushindi. Msingi huu unaweza kujitosheleza kabisa kwa ajili ya ushindi. 

Mahusiano na Mungu yanapimwa kuanzia kiwango cha matumizi yako ya muda. 

 Uliongea na Mungu lini mara ya mwisho wewe peke yako, Kwa sababu yako mwenyewe, au kuhusu biashara yako, au kuhusu ndoa yako, kuhusu mradi wenu, taasisi au jamii yenu..? 

Umetenga muda kwa ajili ya mambo yako yote lakini je Mungu amepata nafasi katika muda wako wa siku? 

Sisemi kwamba Kila siku uende kukusanyika katika ibada, ila nasema kwamba Kila siku unaweza kuwa na muda mfupi wa kuzungumza na Mungu wako. 

Amebarikiwa mtu yule amtegemeaye Bwana, atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya maji.. Mtu anayeboresha mahusiano yake na Mungu ameunganishwa na asili ya mafanikio yake moja kwa moja. Haishiwi, hafilisiki, harusi nyuma kwasababu ameunganishwa na vyanzo vya baraka, ameunganishwa na vyanzo vya ufahamu bora Kwa ajili ya mafanikio yake. ( Mimi ni Mungu nikufundishaye ili upate faida). Taasisi yenye mahusiano na Mungu kadhalika haiwezi kurudi nyuma. 

Kuweka mahusiano mazuri na Mungu ni sawa na kuweka mahusiano na mafanikio yako. 

Wengi hujiuliza nitaanzia wapi au mbona Nina mahusiano mazuri na Mungu. 

Kwa mtu binafsi unaweza kuanza na hii. 

     Kila asubuhi unapojiandaa tenga dakika Tano za kumweleza Mungu kuhusu ratiba yako ya siku husika kisha mwombe akutangulie. Inapofika mchana, angalia dakika tano mueleze kuhusu siku yako jinsi inavyoenda na kumshukuru. Dakika tano tu sio nyingi. Inapofika jioni unaporudi mahali unapojipunzisha, kabla ya mambo mengi, mda mfupi Tena dakika tano mshukuru Mungu kwa siku na tambua aliyokusaidia ukiweza kuandika mahali ni vizuri zaidi. Jikabidhi tena mbele zake kwa muda huo. 

Kwa taasisi kabla ya mambo kuanza, katikati ya siku na baada ya kumalizia siku ifanyike hivyo. Kinachojengeka hapa ni ule utamaduni wa mawasiliano na Mungu. Na ndani yake utamaduni wa ratiba na mpangilio wa siku. Baada ya hapo utamaduni wa kupata mtazamo wa wiki, mwezi hadi Mwaka kuhusu yale uliyokusudia.

Uhusiano wako na Mungu ujikite kumfahamu. Aliwapenda zaidi watu wa namna gani au anafurahishwa na watu gani. Ni kina nani anao wafanikisha.?

Utaona Mungu anawapenda wale wanaompenda, anatokea Kwa wale wanao mtafuta, anawafanikisha wale wanaojibidiisha huku wakintegemea, anawasamehe wale eanaosamehe wengine, anafanya kazi na wale wenye kupenda kumfahamu, anawaongezea baraka wale wenye ufahamu wa kuzimudu au wenye utayari wa kuongeza Maarifa ya kuzimudu baraka hizo. 

Hivyo Kila anayeboresha mahusiano yake na Mungu anaweza kuwa mshindi katika mambo yamuhusuyo. 

Zoezi
Andika mambo kumi uliyofanya siku ya Leo.
Katika mambo hayo, kuna lililojikita kuboresha uhusiano wako na Mungu moja kwa moja? 

2. Uhusiano na watu

Kwasababu huwezi kumpenda Mungu usiye mwona wakati jirani unayemwona unamchukia, na kwasababu Mungu huwatumia watu ili kufanikisha mtu basi ufahamu ukiwa na huduma yeyote unayoitoa kwa jamii au ukihutaji huduma yeyote utahitaji watu. 

Uhusiano wako na watu utakuongezea sifa njema au sifa mbaya.  

Ili uweze kuwa mshindi ni muhimu kujifunza tabia za watu na namna ya kuhusiana nao, kuzifahamu tamaduni zao, maisha yao na mambo wanayoyataka ili uweze kujua ni mpaka gani usivuke na ni wapi hadi wapi ufike bila kuathiri mahusiano Yako na Mungu

Husiana na watu sana kwa kila namna nzuri lakini hakikisha mahusiano yako na Mungu hayaharibiki. 

Sehemu ya tatu . Kudumu kuwa mshindi

Ni rahisi tu, kuendelea kufanya yake yaliyokugikisha katika ushindi ni njia Bora ya kutunza ushindi wako. Bila kusahau kuongeza ufahamu kila mara juu ya namna ya kuendelea kudumu hapo.

Mambo yanayosababisha ushindi kuondoka katika maisha ya mtu, taasisi,familia au jamii.

1. Majivuno. Hali ya kuona kwamba ni kwasababu ya nguvu na juhudi zako au zenu 

Maneno ya kejeli kwa walio chini au ambao hawajafikia hatua hiyo. 

2. Tamaa. Tamaa ya mali au tamaa ya mwili. Kuipa nafasi tamaa kunasababisha mahusiano yaako na Mungu yanaharibika na hivyo mahusiano yako na ushindi wako, huondoa heshima yako kwa jamii yako na hivyo kubandua kidogo kidogo mafanikio yako kama ukoma. 

3. Marafiki/ washauri wabaya. 

Ukikosa ushauri mzuri au watu uliowafungulia moyo wako wakiwa waovu basi jiandae kuelekea njia hiyo hiyo. 

Jitahidi kuepuka marafiki wasio faa kwa gharama zote. 

Usiifiche Imani yako wala usimfiche Mungu wako mana yeye ndiye chanzo cha mafanikio yako. 

Hayo na yanayofanana na hayo yakifanikiwa kuharibu mahusiano yako na Mungu basi ufahamu umepoteza ushindi wako tayari hata kama Bado unaonekana kushinda. 

Mungu akubariki kwa wakati wa kujifunza. 

@David Edwin +255 754 914 944

GHARAMA YA USHINDI

  GHARAMA YA USHINDI 1. Utangulizi 2. Gharama ya ushindi 3. Kudumu kuwa mshindi Sehemu ya kwanza. Utangulizi   Kila jambo unalo ona limekwi...