MBEGU NA MAFANIKIO
Bwana Yesu asifiwe..
Karibu katika siku yetu ya EEMC.
EEMC
ishi kwa malengo, timiza malengo yako.
Mfano wa kwanza.
Machine ya ATM na kadi ya ATM,
Ili utoe hela au upate hela, inabidi uwe na; kadi, Uwezo wa kufikia mashine ya kutoa hela, neno la siri la akaunti husika na pesa kwenye hiyo akaunti.
Tukubaliane Kuwa kila malengo yanamchakato wa kuyatimiza, kama hujaweka mchakato wakuyatimiza inamaana bado hayajawa malengo.
Litambue, lielewe kusudi lako, na kusudi la kufanya chochote ufanyacho.
Purpose,. Kivipi utatimiza malengo?
Tambua majira yako,
Kila mwanadamu anamajira makubwa mawili,
1-Kupanda
2-Kuvuna
Majira haya yana vitu vifuatavyo.
•Kunakuwekeza
•Mbegu
•Kukua
•Akiba
Mbegu
Kila mbegu inamajira yake ya Kupandwa,mahali pa kupanda, na namna ya upandaji.
MAFANIKIO YANATEGEMEA UFAHAMU WAKO JUU YA MAJIRA YA MBEGU ULIYONAYO.
Mtu anayefanya mambo kinyume cha utaratibu ameshindwa kutambua kusudi.
Kuwekeza.
Kuwekeza kwa ajili yako, Take care of your body, kanuni ya kwanza ya uwekezaji ni kuwa na afya nzuri.
Kula vizuri, mwili wako ni sehemu ya kwanza ya uwekezaji.
Weka bajeti nzuri ya kila matumizi yako.
Akiba
Weka akiba kwa ajili ya wakati ujao, itakusaidia kwa ajili ya kesho.
Weka akiba ya kuwekeza kwa ajili ya kesho, ili uweze kufikia malengo ya maisha yako.
Ishi kwa malengo timiza malengo yako.