Sunday, April 14, 2019

Heshimu ibada 2..

         *Mimi na ibada.*

  Muendelezo......
Kanuni ya Ki-Mungu ni kuomba kitu ndo upewe au kifanya kitu ndo ufanyiwe au ukirimiwe kwa kadri ya kunyenyekea/neema,... Hivyo usiende ibadani ukiwa unawaza uko mkamilifu Bali ukiwa na moyo wakuitaji jambo jipya tena na tena,. Moyo wa kushuka ulipondeka maana hao ndo watu Mungu anaowaangalia,.. Nenda na moyo wa toba (najua huna dhambi) lakini toba ni zaidi ya hapo.,
   Nenda ukiwa na shauku na mawazo yako yote kwamba utamuona Mungu Leo na hakika hatokuacha kama ulivyokuja.,
    Usiwe muheshimiwa mbele za Mungu tena wewe muheshimiwa ndo unyenyekee zaidi ,,
   Heshimu ibada.. *huwezi kumsababisha roho ashuke mbele za watu na afanye mambo mapya kama ukiwa mwenyewe hata hashuki, ukiwa mwenyewe hata uneni kwa lugha utawezaje sasa kusema unanena kwa lugha mbele za watu?*
   *Mungu wetu anasifa ya upya kila siku na habadiliki umewahi fikiri hili?*
     Taka jambo jipya kwa Bwana.
     Muheshimu Mungu kwa mavazi yako,. Acha mambo ya kuiga yasiyo tokana na Mungu, ama yaliyo na mashtaka na mashutumu.,(jitahidin kujionesha mmekubaliwa na Mungu)
     Nenda ibadani ukijua ya kuwa unaenda mbele za mfalme wa wafalme,. Kama unaweza kupendeza vizuri Fanya hivyo,. Ila uwe na kiasi sasa,. *Pia soma Walawi 10:10*
  David e k

Saturday, April 6, 2019

Heshimu ibada

*I believe 😊*  Ukianza kuona ibada sio muhimu sana kuliko masomo, kuliko kazi, biashara, n.k ujue kabisa unapaswa kufanya scanning ya iyo roho ngeni iliyokuingia kwa siri.     *#heshimu ibada, nenda ibadani, wahi ibadani, maanisha kuwepo ibadani, vaa kwa heshima ibadani, Fanya ulichokifuata ibadani, muabudu Mungu katika roho na kweli, usitoke kama ulivyoingia Bali utoke na badiliko kwa kupiga hatua zaidi kiroho, kiufahamu, kiafya, kiuchumi, ibada ni zaidi ya kitu muhimu kwako.* @davidek

Thursday, April 4, 2019

Kanuni ya Medali

*Haina maana kwamba wewe usipokua nafasi za juu kihuduma basi usimtafute Mungu, basi usiishi maisha matakatifu laa!!*
   *Nataka nikukumbushe kila kizazi kilikua na wacha Mungu wengi tu kumbuka wakati wa nabiii Yeremia hata manabii wa uongo walikuwepo, sasa unatoka wapi kusingizia msimu huu au kizazi hiki au teknolojia kua sababu ya wewe kutomcha Mungu?*    
     Kama wapo walioinuliwa zaidi yako kihuduma usiwachukie wapende nawewe jitahidi usiwaige ila upate na ufanye kile ambacho Mungu alikuumba ukifanye.
      *Pambana kila Siku hakikisha hakuna kikwazo kitakachokuzuia kufikia malengo na kusudi la Mungu katika maisha yako.*
     *🥇🥇🥇Mimi naiita hii kanuni ya medali,* *🥇🥇🥇  Wewe ni mshindi #1 ukifanya kwa juhudi, kwa malengo, bila kukata tamaa,.*
     
    Nakukumbusha pia unahitaji kujifunza nakuelewa wengine wanafanya nini na sababu za wao kufanya hivyo, lakini katika hili huitaji kujifunza kila kitu Mara moja hapana Bali kwa malengo zaidi na moja baada ya kingine
    *KILA SIKU NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU ITUMIE VIZURI*
   *Fanyia kazi kile kidogo unachofahamu, alafu ongeza uwezo kwa kuongeza ujuzi zaidi*
      *# usipoanza wewe wataanza wengine lakini kamwe hawatafanya kama ambavyo ungefanya wewe#*

   🔐David e kalebi.

WATU WANGU WAJIBU WANGU. MY PEOPLE MY RESPONSIBILITY

 ✓ WATU WANGU WAJIBU WANGU ✓My people my responsibility *NI MUHIMU KUFAHAMU KWAMBA UNATAWAJIBIKA KWA WATU WAKO KATIKA MAMBO YOTE. YAANI YAKI...