Thursday, April 4, 2019

Kanuni ya Medali

*Haina maana kwamba wewe usipokua nafasi za juu kihuduma basi usimtafute Mungu, basi usiishi maisha matakatifu laa!!*
   *Nataka nikukumbushe kila kizazi kilikua na wacha Mungu wengi tu kumbuka wakati wa nabiii Yeremia hata manabii wa uongo walikuwepo, sasa unatoka wapi kusingizia msimu huu au kizazi hiki au teknolojia kua sababu ya wewe kutomcha Mungu?*    
     Kama wapo walioinuliwa zaidi yako kihuduma usiwachukie wapende nawewe jitahidi usiwaige ila upate na ufanye kile ambacho Mungu alikuumba ukifanye.
      *Pambana kila Siku hakikisha hakuna kikwazo kitakachokuzuia kufikia malengo na kusudi la Mungu katika maisha yako.*
     *🥇🥇🥇Mimi naiita hii kanuni ya medali,* *🥇🥇🥇  Wewe ni mshindi #1 ukifanya kwa juhudi, kwa malengo, bila kukata tamaa,.*
     
    Nakukumbusha pia unahitaji kujifunza nakuelewa wengine wanafanya nini na sababu za wao kufanya hivyo, lakini katika hili huitaji kujifunza kila kitu Mara moja hapana Bali kwa malengo zaidi na moja baada ya kingine
    *KILA SIKU NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU ITUMIE VIZURI*
   *Fanyia kazi kile kidogo unachofahamu, alafu ongeza uwezo kwa kuongeza ujuzi zaidi*
      *# usipoanza wewe wataanza wengine lakini kamwe hawatafanya kama ambavyo ungefanya wewe#*

   🔐David e kalebi.

No comments:

Post a Comment

WATU WANGU WAJIBU WANGU. MY PEOPLE MY RESPONSIBILITY

 ✓ WATU WANGU WAJIBU WANGU ✓My people my responsibility *NI MUHIMU KUFAHAMU KWAMBA UNATAWAJIBIKA KWA WATU WAKO KATIKA MAMBO YOTE. YAANI YAKI...