Saturday, September 6, 2025

GHARAMA YA USHINDI

 GHARAMA YA USHINDI

1. Utangulizi

2. Gharama ya ushindi

3. Kudumu kuwa mshindi


Sehemu ya kwanza. Utangulizi 

Kila jambo unalo ona limekwisha fanyika, linafanyika sasa au imepangwa kufanyika baada ya wakati fulani, katika mpango wake Kuna kipengele cha gharama.

Gharama ya jambo inaweza kwa sehemu kubwa kuamua thamani ya Hilo jambo hilo ikishirikiana na matokeo yake. 

Tutajikita zaidi kuangalia gharama ya ushindi katika mambo yamuhusuyo mwanadamu hapa duniani. (Maisha) 

Kwa sababu maisha ni jambo pana lenye tafsiri nyingi nitajitahidi kueleza bila kutumia misamiati migumu na Kwa lugha inayoeleweka. Twende pamoja. . .

Gharama ni aidha muda, nguvu, fedha, mali, maumivu, ufahamu/ujuzi, aina ya maisha, aina ya kazi na mambo yanayofanana na hayo yanayofanyika ili kufanikisha jambo lililokusudiwa Kwa muda mfupi au muda mrefu. 

Mfano wapo watu waliolazimika kuishi maisha ya chini ili wahakikishe wanakamilisha ujenzi, wapo waliolazimika kuongeza ujuzi au kisomo ili wapate aina fulani ya kazi.

Zote hizo ni gharama za ushindi wa Yale waliyo yakusudia. 

Wakati unapanga kufanya jambo au kama hukupanga na umejikuta upo ndani ya jambo, jiulize swali la hili, "ni zipi gharama za jambo hili kufanikiwa?"

Unapozifahamu gharama ni rahisi kuishi kulingana na matakwa ya mafanikio ya jambo lako. 

Wakati mwingine kuzifahamu kunaweza kuhusishwa na woga au hofu juu ya jambo husika, lakini Bado ni muhimu sana kufahamu gharama za kushinda. 

Unapo ona biashara ya mtu inaenda vizuri ujue kabisa kuna gharama ya kusababisha iende hivyo. Unapo ona ndoa ya mtu inaenda vizuri ujue Kuna gharama! Unapo ona maisha ya mtu kidogo yanaenda sawa ujue kuna gharama. 

Kwa lugha nyingine rahisi ki tekinolojia, Kila mara tunachaji vifaa vyetu vya mawasiliano ili kuhakikisha tunaweza aidha kupatikana au kuwapata tunaowatafuta. 

Vivyohivyo tunaweka salio kwenye vifaa hivyo ili tuweze kuwa hewani. Maana yake tumeingia gharama ya kuhakikisha yaliokusudiwa yanafanikiwa. 

Zoezi

1. Andika mambo matatu unayojishughulisha nayo katika maisha yako.

2. Ainisha gharama ya mambo hayo. 


Sehemu ya pili. Gharama ya ushindi 

Kwa kiasi sasa tumeshatambua tunacho kumbushana. 

Zifuatazo ni gharama ambazo zinahusika katika kufanikisha ushindi wa mtu au watu katika jambo lililokusudiwa. 

1. Uhusiano na Mungu. 

Huu ni msingi mkuu wa ushindi. Msingi huu unaweza kujitosheleza kabisa kwa ajili ya ushindi. 

Mahusiano na Mungu yanapimwa kuanzia kiwango cha matumizi yako ya muda. 

 Uliongea na Mungu lini mara ya mwisho wewe peke yako, Kwa sababu yako mwenyewe, au kuhusu biashara yako, au kuhusu ndoa yako, kuhusu mradi wenu, taasisi au jamii yenu..? 

Umetenga muda kwa ajili ya mambo yako yote lakini je Mungu amepata nafasi katika muda wako wa siku? 

Sisemi kwamba Kila siku uende kukusanyika katika ibada, ila nasema kwamba Kila siku unaweza kuwa na muda mfupi wa kuzungumza na Mungu wako. 

Amebarikiwa mtu yule amtegemeaye Bwana, atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya maji.. Mtu anayeboresha mahusiano yake na Mungu ameunganishwa na asili ya mafanikio yake moja kwa moja. Haishiwi, hafilisiki, harusi nyuma kwasababu ameunganishwa na vyanzo vya baraka, ameunganishwa na vyanzo vya ufahamu bora Kwa ajili ya mafanikio yake. ( Mimi ni Mungu nikufundishaye ili upate faida). Taasisi yenye mahusiano na Mungu kadhalika haiwezi kurudi nyuma. 

Kuweka mahusiano mazuri na Mungu ni sawa na kuweka mahusiano na mafanikio yako. 

Wengi hujiuliza nitaanzia wapi au mbona Nina mahusiano mazuri na Mungu. 

Kwa mtu binafsi unaweza kuanza na hii. 

     Kila asubuhi unapojiandaa tenga dakika Tano za kumweleza Mungu kuhusu ratiba yako ya siku husika kisha mwombe akutangulie. Inapofika mchana, angalia dakika tano mueleze kuhusu siku yako jinsi inavyoenda na kumshukuru. Dakika tano tu sio nyingi. Inapofika jioni unaporudi mahali unapojipunzisha, kabla ya mambo mengi, mda mfupi Tena dakika tano mshukuru Mungu kwa siku na tambua aliyokusaidia ukiweza kuandika mahali ni vizuri zaidi. Jikabidhi tena mbele zake kwa muda huo. 

Kwa taasisi kabla ya mambo kuanza, katikati ya siku na baada ya kumalizia siku ifanyike hivyo. Kinachojengeka hapa ni ule utamaduni wa mawasiliano na Mungu. Na ndani yake utamaduni wa ratiba na mpangilio wa siku. Baada ya hapo utamaduni wa kupata mtazamo wa wiki, mwezi hadi Mwaka kuhusu yale uliyokusudia.

Uhusiano wako na Mungu ujikite kumfahamu. Aliwapenda zaidi watu wa namna gani au anafurahishwa na watu gani. Ni kina nani anao wafanikisha.?

Utaona Mungu anawapenda wale wanaompenda, anatokea Kwa wale wanao mtafuta, anawafanikisha wale wanaojibidiisha huku wakintegemea, anawasamehe wale eanaosamehe wengine, anafanya kazi na wale wenye kupenda kumfahamu, anawaongezea baraka wale wenye ufahamu wa kuzimudu au wenye utayari wa kuongeza Maarifa ya kuzimudu baraka hizo. 

Hivyo Kila anayeboresha mahusiano yake na Mungu anaweza kuwa mshindi katika mambo yamuhusuyo. 

Zoezi
Andika mambo kumi uliyofanya siku ya Leo.
Katika mambo hayo, kuna lililojikita kuboresha uhusiano wako na Mungu moja kwa moja? 

2. Uhusiano na watu

Kwasababu huwezi kumpenda Mungu usiye mwona wakati jirani unayemwona unamchukia, na kwasababu Mungu huwatumia watu ili kufanikisha mtu basi ufahamu ukiwa na huduma yeyote unayoitoa kwa jamii au ukihutaji huduma yeyote utahitaji watu. 

Uhusiano wako na watu utakuongezea sifa njema au sifa mbaya.  

Ili uweze kuwa mshindi ni muhimu kujifunza tabia za watu na namna ya kuhusiana nao, kuzifahamu tamaduni zao, maisha yao na mambo wanayoyataka ili uweze kujua ni mpaka gani usivuke na ni wapi hadi wapi ufike bila kuathiri mahusiano Yako na Mungu

Husiana na watu sana kwa kila namna nzuri lakini hakikisha mahusiano yako na Mungu hayaharibiki. 

Sehemu ya tatu . Kudumu kuwa mshindi

Ni rahisi tu, kuendelea kufanya yake yaliyokugikisha katika ushindi ni njia Bora ya kutunza ushindi wako. Bila kusahau kuongeza ufahamu kila mara juu ya namna ya kuendelea kudumu hapo.

Mambo yanayosababisha ushindi kuondoka katika maisha ya mtu, taasisi,familia au jamii.

1. Majivuno. Hali ya kuona kwamba ni kwasababu ya nguvu na juhudi zako au zenu 

Maneno ya kejeli kwa walio chini au ambao hawajafikia hatua hiyo. 

2. Tamaa. Tamaa ya mali au tamaa ya mwili. Kuipa nafasi tamaa kunasababisha mahusiano yaako na Mungu yanaharibika na hivyo mahusiano yako na ushindi wako, huondoa heshima yako kwa jamii yako na hivyo kubandua kidogo kidogo mafanikio yako kama ukoma. 

3. Marafiki/ washauri wabaya. 

Ukikosa ushauri mzuri au watu uliowafungulia moyo wako wakiwa waovu basi jiandae kuelekea njia hiyo hiyo. 

Jitahidi kuepuka marafiki wasio faa kwa gharama zote. 

Usiifiche Imani yako wala usimfiche Mungu wako mana yeye ndiye chanzo cha mafanikio yako. 

Hayo na yanayofanana na hayo yakifanikiwa kuharibu mahusiano yako na Mungu basi ufahamu umepoteza ushindi wako tayari hata kama Bado unaonekana kushinda. 

Mungu akubariki kwa wakati wa kujifunza. 

@David Edwin +255 754 914 944

Tuesday, May 6, 2025

WATU WANGU WAJIBU WANGU. MY PEOPLE MY RESPONSIBILITY

 ✓ WATU WANGU WAJIBU WANGU

✓My people my responsibility

*NI MUHIMU KUFAHAMU KWAMBA UNATAWAJIBIKA KWA WATU WAKO KATIKA MAMBO YOTE. YAANI YAKIWA YA FURAHA AU YA HUZUNI LAZIMA KUNA NAMNA YATAKUHUSU

It's important to understand that you'll be responsible for your people in everything. If they mourn or they celebrate in one way or another you'll be involved. 

*IKIWA UTASIMAMA KWA UAMINIFU NA KATIKA MAJUKUMU YAKO YOTE BILA KUONA HAYA BASI WATU WAKO WATAKUA SALAMA WAKIISIKIA SAUTI YA MUNGU KUPITIA KWAKO.

If you'll faithfully stand and in all your responsibility may be (as a leader/father), your people will be safe if they'll listen to the voice of God as He speaks through you.

*INAWEZA TOKEA BAADHI YAO WASIKUSIKILIZE, HAO WATAPATA HASARA KUBWA! SIO YA MALI TU HUENDA HATA MAISHA YAO. 

It might happen that they don't listen to you . They'll have great loss not only of material things or wealth but even their lives. 

*KAMA JAMBO BAYA LITATOKEA MAHALI NA MCHA MUNGU YUPO NA IKAWA KIMYA AU BILA TAARIFA BASI KUNA MAMBO HAYAKUKAA SAWA. 

If a bad thing will happen at a certain place and a righteous man/woman  is there without any information, something will be  probably wrong somewhere. 


* KAMA UKISIMAMA KATIKA NAFASI YAKO KWA UAMINIFU, BASI UFAHAMU YA KWAMBA UTALETA USALAMA SIO WAKO TU HATA WA WATU WAKO. (WALE WATAKAO SIKIA NA KUKUBALI KUTII)


If you faithfully stand at your position, you and your people will be safe but only if they'll listen and accept the truth. 


*MWANZO 19:12

*BASI WALE WATU WAKAMWAMBIA LUTU, JE! UNAYE MTU HAPA ZAIDI? MKWE, WANAO, NA BINTI ZAKO, NA WO WOTE ULIO NAO KATIKA MJI, UWATOE KATIKA MAHALI HAPA;


Genesis 19:12

And the men said unto Lot, Hast thou here any besides? son in law, and thy sons, and thy daughters, and whatsoever thou hast in the city, bring them out of this place:

ILI YATOKEE SHUGHULIKIA USIKU. DEALING WITH THE NIGHT TO BRING OUT RESULTS

ILI YATOKEE, SHUGHULIKIA USIKU


Dealing with the night to bring out results. 


•MAJIRA YALE AMBAYO ADUI ANAFIKIRI UMELALA HAPO NDIPO UNA AMKA NA KUIDAI HATMA YAKO MIKONONI MWA ADUI. 

When the enemy thinks you are asleep, it's when you rise and claim your destiny from the hands of your enemy. 

•KAMA MTOTO WA MUNGU UNAONA KUNA JARIBU LIMEKUKARIBIA USIHANGAIKE HUKU NA KULE. AU KULALAMIKA AU KULAUMU HAPANA!

As a child of God, whenever you find your self in temptation, don't begin to lament or deal with it like how others do.. No!

•AMKA USIKU IANDIKE HIYO HALI, HILO JARIBU, HUO MSIBA, HICHO KILIO, HAKIKISHA UNAKIANDIKA KWA MAPANA YAKE. 

Get up in the night, write that issue down, that pain, that cry and any sort of challenge you are through. Analyze it properly 

•USIZUNGUMZE NA WATU WENGI ANZA KUFANYIA KAZI. INGIA KWENYE MAOMBI.

Don't try to share it with many people.. just pray!! 

•KUNA BAADHI YA WATU UNAWEZA KUWAELEZA KUMBE WANAHUSIKA NA HALI UNAYOIPITIA.

Because some of the people you share with might be responsible with what you are going through.

•USIPO AMKA ADUI WALA HANA HURUMA. 

If you won't get up the enemy is merciless. 

•USIPO AMUA ADUI ATAENDELEA KUZOEA KUKUCHEKA.

If you don't decide the enemy will continue to mock you. 

NEHEMIA 2:12

KISHA NIKAONDOKA USIKU, MIMI NA WATU WACHACHE PAMOJA NAMI; WALA SIKUMWAMBIA MTU NENO HILI ALILOLITIA MUNGU WANGU MOYONI MWANGU, NILITENDE KWA AJILI YA YERUSALEMU; 


Nehemiah 2:12

And I arose in the night, I and some few men with me; neither told I any man what my God had put in my heart to do at Jerusalem: 

Thursday, January 2, 2025

MAMBO YA MUHIMU 2025

Namshukuru Mungu Kwa kutuvusha tena Kwa ushindi mwaka huu. 

Utangulizi

Wakati najiandaa na kumuomba Mungu juu ya Yale ninayotamani kuyafanya Mwaka 2025, Roho mtakatifu alinielekeza pia kuomba ili nifahamu Mungu amekusudia jambo gani kwangu Mwaka huu.

#. Kwanza kabisa, ni vizuri kuwa na mipango lakini ni muhimu kufahamu kwamba Mungu anayo mipango yake pia kulingana na majira ya maisha Yako.

Naona una malengo yako lakini Je! unayafahamu malengo ya Mungu juu Yako?

Utayafahamuje? nenda kwenye kikao barazani pa Bwana. Tenga muda mchache wa muhimu wa kuyaombea hayo uliyopanga na atakuambia lipo litafanyika na lipi lianze Tena Kwa namna gani lianze. Kina nani ushirikiane nao n.k na kama asipo kupambia Kwa sauti ataruhusu ufahamu uhalisia wa watu unaoshirikiana nao ili aweke umakini ndani yako wa namna ya kufanya nao kazi. 

Anaweza pia kuruhusu usome kitabu muhimu au uhudhurie semina itakayo fungua mawazo na ufahamu wako juu ya Hilo jambo.

Mambo Muhimu 

1. Mahusiano na Mungu. 

Unafanya kazi kubwa sana kuzitafuta nguvu za Mungu kuliko kazi ya kuzilinda

 Hii ni hatari kwako kwasababu ni sawa na mtu anayetafuta Mali Kwa gharama kubwa alafu anazitunza kwenye nyumba isiyo fungwa milango. Utapoteza muda mwingi, bila matokeo unayoyataka. Kuna mambo yatahitaji mahusiano yako na Mungu kuwa mazuri ili yatokee bila kutumia nguvu kubwa. 

Yakobo 4:8 (Kumkaribia Mungu naye kutukaribia)  

Kama utalinda kile unachopokea kwenye ibada ya katikati ya wiki au ibada ya jumapili basi kufunga na kuomba kitakua ni Kwa ajili ya Yale mengine yasiyowezekana isipokuwa Kwa kufunga na kuomba. 

Ameniambia hakuna maana ya kukesha kumwomba Mungu alafu huwezi kukesha kulinda ulimi wako, kulinda moyo wako, kulinda mawazo Yako, macho Yako n.k 

Lazima uelewe kwamba nguvu za Mungu unazopokea ni za thamani sana usizipoteze kihivi hivi tuu. 

2. Matumizi ya muda 

Muda wako wa thamani unautumiaje?

Mfano mrahisi, simu yako vs bibilia Yako. Najua simu ina bibilia pia. Na simu ina vitabu. Ila pia simu ina TikTok, fb, insta, na hata huko unaweza pata mambo ya kuongeza thamani.  Suala kubwa ni kuwa makini na matumizi ya muda wako na juu ya kufahamu je hili ninalolifanya hapa linaniongezea thamani au linaniongezea changamoto?

Kama Mwaka huu utatumia muda mwingi kwenye mambo yasiyo kuongezea thamani basi jiandae kupunguza kiwango cha ufaulu wa mipango yako.


Badala ya kujua nani amefanya Nini, unaweza kujikita kujifunza mambo mapya au kuongeza ujuzi kwenye Yale unayoyafanya kupitia hiyo hiyo simu yako. 

Sina ugomvi na simu ila, nakukumbusha uwe (specific) na kile  unachokifanya kwenye simu yako. 

Kina matokeo gani kwako? Ukikuta matokeo hayakufai achana nacho. 

Nitaendelea. 


3. Mahusiano na Watu. 

Ni wazi kwamba watu ndio huinua watu wengine, lakini pia Watu ndio wanaoweza kukushusha. Napenda kurejea baadhi ya maneno ya kiongozi wetu mkuu katika nchi Mhe. Samia Suluhu Hassan, "Watu ni mashahidi wa Mungu".  

Mwaka huu jitahidi sana kuwa na mahusiano rafiki kwa ajili ya hatma yako. Utafanikiwaje? 

Kwanza yale unayopenda kufanyiwa, wafanyie wengine. Usipoteze muda na watu ambao hawaongezi thamani katika maisha yako. Sijasema uwadharau, hapana!!  Sijasema uwapuuzie, hapana ila linda sana matokeo wanayoweza kuya leta kwako mnapokuwa pamoja nao. 

Tafuta ukaribu na watu wenye ndogo kubwa, watu wenye maono makubwa, bila kuwadharau hawa wadogo. 

Mwaka huu mtu asiye na matokeo asikushauri! Unaweza kusikiliza hekima zake ila usiziweke moyoni mana mara nyingi kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake. 

Katika kuhusiana na watu, tengeneza thamani yako, watu sahihi watavutika kwako. Ni vizuri kutumia nguvu kuwatafuta watu wapya lakini ni vizuri zaidi kuboresha vile ulivyo mana watu wa thamani watakutafuta tu!. 

Unaboreshaje? Unavaaje kama mtu mwenye safari ya ukuu au kama watu wa kawaida? Unazungumzaje? Unashiriki kwa namna gani kwenye mambo ya wengine, vipi matumizi yako ya fedha(tuytaizungumzia zaidi hii pia), ushiriki wako kwenye jamii iliyopo karibu nawewe je? 

Mtu akikusikiliza Kwa dakika kumi anaweza kufahamu ni mtu wa namna gani. Kichwani kwako umeweka vitu gani? Njia ya mwanzo ya kujiongezea thamani ni kuongeza ufahamu wako. 

Tafuta eneo moja ambalo unalipenda au unalifanyia kazi alafu ujikite kuongeza ufahamu katika hilo eneo, japo sio lazima liwe eneo lako la kiutaalamu.  

4. Nidhamu ya fedha.  

Unapenda kutumia kiwango ambacho hakiendani na kiasi unachoingiza. 

Nidhamu ya fedha inaendana na ufahamu sahihi wa elimu ya umiliki wa fedha ambayo mara nyingi haifundishwi shuleni. 

Unaweza kujifunza Kwa watu waliofanikiwa au kupitia vitabu vingi ambavyo vimeeleza juu ya nidhamu ya fedha au namna ya kuimiliki. 

Kwa kifupi tu mwaka huu kama hujaorodhesha mipango yako bado, unahutaji kukaa na kufanya hiyo kazi. Na mpango wa kwanza uwe kuweka akiba ya angalau matumizi yako ya miezi mitatu. 

Maana yake hapo uweke kiasi Cha pesa ambacho utakua na uhakika wa kuendelea kuishi Kwa miezi mitatu mfululizo hata usipo pata ingizo lolote jipya la kipato Kwa muda huo. 

Hii inakupeleka moja kwa moja kwenye bajeti. Unaijua bajeti yako ya mwezi? Hii inakulazimisha utafute kufahamu ratiba ya matumizi, chakula, safari n.k 

Tabia ya kutumia kwasababu vipo, au kupooza moyo kama wanavyodai wengine imesababisha watu wakachukulia poa fursa walizokutana nazo ambazo zingebadilisha maisha yao. 

Hii ndiyo sababu unaweza kumkuta mtu asiye na kipato maalum akifanya maendeleo wakati mwenye kazi na kipato maalum akiwa hajafanya chochote. 

Mfano mdogo

Ukinunua simu ya milioni moja wakati unauwezo wa kununua ya milioni tatu, huo ni ufahamu wa kiuchumi. 

Lakini..

Ukinunua simu ya milioni moja wakati uwezo wako ni wa kununua ya milioni moja, hilo ni kosa la kiuchumi. 

Haya sio maneno mageni mjini, labda Kwa mgeni mjini. Mwaka huu tujifunze sana namna ya kumudu fursa zinazopita mikononi mwetu, ili tusije kufika mwisho na majuto ya kutokufanya vizuri. 

Nitaendelea. . 







  

Tuesday, March 28, 2023

THE GOOD WINE 🍷

THE GOOD WINE  🍷
John 2:10
And saith unto him, Every man at the beginning doth set forth good wine; and when men have well drunk, then that which is worse: but thou hast kept the good wine until now.

Shalom brethren!
I wanna speak a little bit about
 "THE GOOD WINE" 
 As from our reference.. There's a norm that people are used to. There's a traditional practice of doing or handling things. 
Traditionally there are double standards. If not with economic aspect then age, if not age, then popularity, position/authority, gender, tribal, region/origin and any other phenomena that can be used to group people.

Have you ever walked to a parking with reservations? What about an event with seats reserved for so and so...
So let's go now..
1. At the beginning.•°••°•
 External appearance of something,. Before understanding the innermost characters of something/someone. 
Before getting into it
Before you start that ministry 
Before you start that behavior/lifestyle
Before you get into that crew of gamblers
Before you begin to pursue her/him
Before you start going for your dreams/purpose 
Every man at the beginning doth set good wine..


2. And when men have well drunk..° °•°•°•°
After you get what you thought you saw, or needed. After you've achieved getting her heart/his affection. 
After you've married her/him
After you've got into something you thought it was pleasant/ that would give you joy/peace/ pleasure 
When you've now come to a place of achievement
When you've now successfully managed your credits
When you've got all you wanted/prayed for.

3. Then that which is worse is brought°•°•°°••°•••
When the ups and downs arise a real character mist show up
When temptations rise some people astray from from the will of God.
Some forget or neglect the standards after achieving their goals. 
They don't offer the best service again.
No longer available in church service.
Not humble as in the beginning.. they've got what they wanted.
Not hardworking anymore
They are not ready to serve again, love again or cherish their spouses. They've arrived where they wanted to.
Now you're with the real person
With the original somebody
No more camouflages 
You can only see the true colors.
 
4. But thou hast kept the good wine until now. 🍷
What does keeping good wine until now mean? 

Maintaining the standards of..
Quality
Holiness 
Righteousness
Hard working
Love
Concern
Care
Humbleness
Wisdom
Humility
The outside you being the same as the inside you
Character etc...

Generally can we just conclude it as Taste/ Ever-tasty

Qn. How can this be achieved?
Here's a clear simple way to make it.
Jesus did a miracle He turned water into fine/good/standard wine.
What ever you need/you've been through in your life, just repent and pray this short powerful prayers with me. 
   Jesus, I believe that you are the son of God, and that you gave your life on the cross that I may have everlasting life. 
Please forgive all my sins and make me whole again.
In Jesus name I pray. Amen

Dear brethren. What you've done is now like filling  your water pots with water. Jesus is going to turn that water into fine-good wine. 

Be blessed as you live a life of testimonies in Jesus name. 
EVER-TASTY

Saturday, March 25, 2023

THE HEART OF ENQUIRY

Greetings in the name of our Lord and savior Jesus Christ.
Today I want to share a word of God with the tittle, "THE HEART OF ENQUIRY" 
May we pray Before we begin. 
Father in the mighty name of Jesus. We thank you for giving us this opportunity to share your word. Your word is life Dear God. May it reform our spirits to your will,  rekindle the fire in us, bring hope and revive the inner man. In the name of the father, the son and the holy spirit we pray. Amen.

SHALOM!!! 
 Scripture Reference. 
1 Samwel 30:8
2 Samwel 2:1
2 Samwel 5:19

Questions to be answered as you take your time to study this short lesson.
1. Can I really enquire of the Lord.
2. Is it necessary to enquire of the Lord.
3. What does enquire of the Lord imply?
And many more questions as the Spirit of God will be taking you through the lesson. 
Once again you are welcome.

2 Samwel 2:1 
And it came to pass after this, that David enquired of the LORD, saying, Shall I go up into any of the cities of Judah? And the LORD said unto him, Go up. And David said, Whither shall I go up? And he said, Unto Hebron.

Shall I go... Many are times that we move without permission but just because we think we can move. 
Sometimes we can really do it but sometimes the Lord has the best way to do it and its were we need to enquire. Basically we need to totally depend on Him. Enquiring is kind of submission onto the Lord. 
We don't willingly enquire unless we are able and ready to obey what He says. 
Enquiry is very important in times of great challenges.
As a servant of God, an ambassador of His Kingdom, a partaker of His Kingdom or a child of God, you really need a heart that asks from the Lord. 
CHOICES
When you've got choices. But you really can't figure out which one should start. 
You can't win in battles by depending only on your understanding. It is impossible to make it by your own counsel. Unless the Spirit of God is advising you in the inside about something that is going on. 

You can begin this by letting your thoughts align with the word of God and the will of God. Easily will your actions prove and glorify God.
Victory
You get assurance of victory through enquiry... 

The heart of Enquiry give God the glory.
Thank you may I end up here. Be blessed as you receive this message. 

Ref. 
1 Sam 30:8
And David enquired at the LORD, saying, Shall I pursue after this troop? shall I overtake them? And he answered him, Pursue: for thou shalt surely overtake them, and without fail recover all.
Judges 20:27
And the children of Israel enquired of the LORD, (for the ark of the covenant of God was there in those days,


#David Edwin 



Wednesday, December 16, 2020

Kumtumaini Bwana.

Kumtumaini Bwana. Hope in the Lord
Yeremia 10;23
Mithali 16:9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake.
A man's heart deviseth his way: but the LORD directeth his steps.

Mwana wa Mungu jifunze kumtegemea Mungu maana yeye ndiye kilakitu

Kumtumaini Mungu kunaweka nanga katika maisha yako, ni kuweka msingi bora wa maisha yako...
Yesu ni nanga imara.
Kumtumaini Mungu ni nanga imara.

Zifahamu roho chafu zinazoweza kumuingia mtu.

Unclean spirits zinaudhi, kama zimekuudhi unahitaji uponyaji kabisa.  Unapomuona mtu ameanza maudhi maudhi ana asilimia kadhaa za roho chafu kuwa ndani yake, Je mtu anaweza kuwa na mapepo na yasijioneshe?(manifest): ndio lakini anapo kaa au anapokutana na uwepo wa nguvu za Mungu zinaleta madhara kwahivyo hizo roho chafu zinajidhihirisha au zinaweza kumuamrisha aondoke eneo hilo.
Nguvu zikiendelea kumuishia basi ile roho chafu humtoka

Saturday, November 2, 2019

How to deal with the death letter. Namna ya kushughulikia waraka/barua ya mauti.

A letter is a formal/informal script to demand for an opportunity, to give instructions and to give good or bad news. 
You can define it in many other ways but let's get this brief. 
Who writes a letter? Anyone can write a letter according to the rank he/she is writing from. Spiritual or physical letters have stamps in which the stamps are defined by the authority of the respective association,  group, nation etc.
 A letter can be written as an information to uplift you or fire you from work. It can be written by the great authorities to shift you or demand something from you.
It can be written to abuse you or call you to war. 
A letter can be the way nations and kingdoms communicate. 
Uriah was sentenced to death through a letter. Am not much interested with the origin cause of his death now but I have just made up a thought that; what if he captured the letter? What if that letter didn't reach Yoab?
Definetly his death wouldn't happen by that time. 
Many are times that we are sentenced to destructions and o yet we even don't know what's going on. 
May the Lord give you the grace/strength to destroy the evil letters against us in Jesus name.

Scripture reference.
2 Samweli. 11:15
 Akaandika katika waraka huo, kusema, Mwekeni Uria mbele ya watu penye vita vikali, kisha ondokeni, mmwache, ili apigwe akafe.

2 Samwel 11:15
And he wrote in the letter, saying, Set ye Uriah in the forefront of the hottest battle, and retire ye from him, that he may be smitten, and die.
Read more..
2 Chronicles 32:17

Prayer work out!
Destroy every letter written by any evil purpose against you destiny in Jesus mighty name. 
And if you are unable do what Hezekiah did,
Ref... 
Spread that letter before the Lord!
Isaiah 37:14
Basi Hezekia akaupokea waraka katika mikono ya wale wajumbe, akausoma; kisha Hezekia akapanda, akaingia katika nyumba ya Bwana, akaukunjua mbele za Bwana.
And Hezekiah received the letter from the hand of the messengers, and read it: and Hezekiah went up unto the house of the LORD, and spread it before the LORD.

Yes they abused you, they spoke lies on you, just write down what they said and spread it before the Lord.  
May the Lord intervene your sistuation in Jesus mighty name.. Have a blessed moment .


Thursday, October 17, 2019

Siri ya kujazwa nguvu kila wakati. The secret of being filled with power all the time.

Bwana Yesu asifiwe!
Praise the be to Jesus!
I want we take a short time to the secrets of being filled with power ( holy spirit power) all the time.
Nataka tuchukue muda mfupi kuangalia siri za kujazwa nguvu ( nguvu za roho mtakatifu) kila wakati.

Tutazame maandiko...
Let's see the scriptures....

Marko 1:35
Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.

Mark 1:35
And in the morning, rising up a great while before day, he went out, and departed into a solitary place, and there prayed.

Tunamuona Yesu akiondoka alfajiri na mapema kujitenga mahali na kuomba.
-(Asubuhi na mapema = Inaonesha kitu cha kwanza kabisa na cha thamani)
-(Mahali pasipokuwa na watu= Inaonesha utulivu na kujitenga mbali na kila mawazo na fikra za tofauti zozote)
-(Kuomba=Inaonesha kumwitaji Mungu na kunyenyekea kwake)

We see Jesus departing in early morning to a solitary place and praying.
-(Early morning=Shows the first valuable thing)
-(Solitary place=Shows a quite place away from any disturbances and every disturbing thoughts)
-(Praying=Shows the humbled heart and one in need of God's assistance)

So before we take a leap to other secrets lets take a close look on to this one as a question..
Do you have time to refuel/refill and strengthen your spirit?
Yes you fasted last week but God has new things for you everyday!
  Take time to a solitary place severally and your connection with the Holy spirit will be strong his powers will be coming out from you every time.

Hivyo kabla ya kupiga hatua kuangaliasiri zingine, tuangalie hii moja kama kwa swali...
Je una muda wako wa kujiimarisha? Na kuimarisha mahusiano yako na Mungu?
Ndio ulifunga wiki Jana lakini kumbuka Mungu anamambo mapya kwa ajili yako kila siku.
Chukua hatua uwe na muda wa kujitenga Mara kwa Mara na muunganiko wako na roho mtakatifu yataimarika sana zaidi nguvu zake zitatoka ndani yako kila siku kila saa..

Other secrets
-The word of God
Siri zingine
-Neno la Mungu

Be blessed as you follow.....
Ubarikiwe unavyozidi kufuatilia....

Why publishing everything to everyone? Kwanini utangaze kila kitu kwa kila mtu?

Should I publish and blaze about everything that God has done for me?
Je ni lazima nitangaze na niseme kila kitu alichonitendea Mungu?
Praise be to the Lord Jesus Christ!! Bwana Yesu Kristo asifiwe!!

Tunaishi katika dunia yenye mapambano mengi na vita vilivyojificha sana. Ni muhimu sana kushudia yale mambo Mungu amekutendea, lakini sio sheria ushuhudie kila kitu. Kumbuka sio watu wote wanaokusikiliza wanayafurahia hayo hivyo sababu hii inatupa msingi wa kuwa na kiasi katika kushuhudia/ kuyasema yale ambayo Mungu ametutendea.
We live in a world with so much wars and hidden battles. Yes it is important to share and publish the things that God has done for us yet its not necessarily a law that you must share everything.
Remember that not everyone that listens to you are happy and comfortable about what you share and publish. Then this gives us a foundation of the measure what we should share and what we shouldn't.
What do you share with whom do you share and when do you share!
Look at the scriptures....
Tazama maandiko....

Marko 1:44.              
akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.

Mark 1:44
And saith unto him, See thou say nothing to any man: but go thy way, shew thyself to the priest, and offer for thy cleansing those things which Moses commanded, for a testimony unto them.

Why speaking out everything?
Kwa nini utangaze kila kitu?
         Je, utapata hasara gani au madhara gani katika hayo uyasemayo?

        What are the effects of publishing or sharing what you shouldn't share?

Let's take a look at the scriptures again...
Tuangalie maandiko tena....

Marko 1:45

Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwako nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila mahali.

Mark 1:45

But he went out, and began to publish it much, and to blaze abroad the matter, insomuch that Jesus could no more openly enter into the city, but was without in desert places: and they came to him from every quarter.

-We see here that Jesus could no longer enter the city openly.
-Tunaona hapa Yesu hakuweza tena kuingia mjini kwa wazi.

Its your time to evaluate your self, how many opportunities have you blocked out yourself by publishing everything, every time to everyone?, how many enemies have you increased through sharing what you were not supposed to share?

Ni muda wako wakujitathmini sasa, Ni fursa ngapi umejizibia kwa kutangaza kila kitu, kila Mara kwa kila mtu?, ni maadui wangapi umeongeza kwa kushirikisha na kutangaza yale ambayo hukupaswa kutangaza?

Be blessed as you continue following the word of life.
Ubarikiwe kama unavyoendelea kufuatilia neno la uzima.

Wednesday, October 16, 2019

MBEGU NA MAFANIKIO

MBEGU NA MAFANIKIO
Bwana Yesu asifiwe..
        Karibu katika siku yetu ya EEMC.
                           EEMC
ishi kwa malengo, timiza malengo yako.
Mfano wa kwanza.
Machine ya ATM na kadi ya ATM,
Ili utoe hela au upate hela, inabidi uwe na; kadi, Uwezo wa kufikia mashine ya kutoa hela, neno la siri la akaunti husika na pesa kwenye hiyo akaunti.

Tukubaliane Kuwa kila malengo yanamchakato wa kuyatimiza, kama hujaweka mchakato wakuyatimiza inamaana bado hayajawa malengo.

Litambue, lielewe kusudi lako, na kusudi la kufanya chochote ufanyacho.

Purpose,. Kivipi utatimiza malengo?
Tambua majira yako,
Kila mwanadamu anamajira makubwa mawili,
1-Kupanda
2-Kuvuna
Majira haya yana vitu vifuatavyo.
•Kunakuwekeza
•Mbegu
•Kukua
•Akiba
Mbegu
Kila mbegu inamajira yake ya Kupandwa,mahali pa kupanda, na namna ya upandaji.

MAFANIKIO YANATEGEMEA UFAHAMU WAKO JUU YA MAJIRA YA MBEGU ULIYONAYO.

Mtu anayefanya mambo kinyume cha utaratibu ameshindwa kutambua kusudi.

Kuwekeza.
Kuwekeza kwa ajili yako, Take care of your body, kanuni ya kwanza ya uwekezaji ni kuwa na afya nzuri.
Kula vizuri, mwili wako ni sehemu ya kwanza ya uwekezaji.
Weka bajeti nzuri ya kila matumizi yako.
Akiba
Weka akiba kwa ajili ya wakati ujao, itakusaidia kwa ajili ya kesho.
Weka akiba ya kuwekeza kwa ajili ya kesho, ili uweze kufikia malengo ya maisha yako.
    
     Ishi kwa malengo timiza malengo yako.

Wednesday, August 14, 2019

Confidence and Courage "Ev. Bernard Selemani.

What is your confidence??

Courage or Strength -
Means the heart to go on,
The mindset to dare
The faith towards your belief
The power to hold on despite of the challenge

1 Sam 17:31
Confidence means belief in your ability. Trusting that you can make it despite of the situation.

David a young man who was spirit filled had a courage and was confident to face Goliath with a strong determination of victory because he understood who/where his strength were from...
  He gives some experience about several trials that came his way as a Father's shepherd and compares to the current trial and gets a great assurance of victory...
How does confidence come?
Confidence comes through...
1-Understanding who is within you. Acknowledge Your God !!!

2-Being righteous-doing what is right before God, this will give you favour before God moreover it will enhance your prayer/communication with God.
Living righteous life assures you of the power of God within you.
Sin draws away confidence.

Have you lost the courage,? Here is a second chance.
God is calling for your heart back to him again!
Running away from salvation won't help you get that courage and confidence back but either it will destruct you completely.

Change your mind, come back to the cross

Yes you have been abandoned, yes you have messed up a lot.!.
It is enough Get up again and God will rebuild your strength within seconds of your decision.

As a believer make sure that you do what God said and if in anyway you are weak keep in mind that any weakness you got is not a guarantee for you to miss attend any program or calling that God has placed on you.

Let your Courage and strength be restored in Jesus mighty name

    ............  AMEN ................

Thursday, August 1, 2019

MBEGU NA MAFANIKIO

MBEGU NA MAFANIKIO
Bwana Yesu asifiwe..
        Karibu katika siku yetu ya EEMC.
                           EEMC
ishi kwa malengo, timiza malengo yako.
Mfano wa kwanza.
Machine ya ATM na kadi ya ATM,
Ili utoe hela au upate hela, inabidi uwe na; kadi, Uwezo wa kufikia mashine ya kutoa hela, neno la siri la akaunti husika na pesa kwenye hiyo akaunti.

Tukubaliane Kuwa kila malengo yanamchakato wa kuyatimiza, kama hujaweka mchakato wakuyatimiza inamaana bado hayajawa malengo.

Litambue, lielewe kusudi lako, na kusudi la kufanya chochote ufanyacho.

Purpose,. Kivipi utatimiza malengo?
Tambua majira yako,
Kila mwanadamu anamajira makubwa mawili,
1-Kupanda
2-Kuvuna
Majira haya yana vitu vifuatavyo.
•Kunakuwekeza
•Mbegu
•Kukua
•Akiba
Mbegu
Kila mbegu inamajira yake ya Kupandwa,mahali pa kupanda, na namna ya upandaji.

MAFANIKIO YANATEGEMEA UFAHAMU WAKO JUU YA MAJIRA YA MBEGU ULIYONAYO.

Mtu anayefanya mambo kinyume cha utaratibu ameshindwa kutambua kusudi.

Kuwekeza.
Kuwekeza kwa ajili yako, Take care of your body, kanuni ya kwanza ya uwekezaji ni kuwa na afya nzuri.
Kula vizuri, mwili wako ni sehemu ya kwanza ya uwekezaji.
Weka bajeti nzuri ya kila matumizi yako.
Akiba
Weka akiba kwa ajili ya wakati ujao, itakusaidia kwa ajili ya kesho.
Weka akiba ya kuwekeza kwa ajili ya kesho, ili uweze kufikia malengo ya maisha yako.
    
     Ishi kwa malengo timiza malengo yako.

Monday, July 22, 2019

UAMINIFU

                         UAMINIFU.
BWANA YESU ASIFIWE!!
Na Mwl....
.....Karibu katika somo letu la uaminifu.....

Mwisho wa somo hili utaweza kujijibu maswali haya na mengine mengi.

Uaminifu ni nini?
Mimi ni mwaminifu?
Je ninahitaji kuwa mwaminifu?
Inawezekana nikakosa uaminifu?
Je nahitaji uaminifu katika mambo gani?

Tuanze kuangalia haya.
Soma Mathayo 25:14 ..
Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
And unto one he gave five talents, to another two, and to another one; to every man according to his several ability; and straightway took his journey.

Ni wapi/kivipi tunapaswa kuwa waaminifu?
(A) Kuwa waaminifu mbele za Mungu,
  1Korintho 1:9
  1Korintho 4: 1-2
   Torati 7:9
Mungu Mwenyewe ni mwaminifu na yeye ni chanzo cha uaminifu

(B) Kuwa waaminifu kwa watu wengine.
Mathayo 24:45-47 Kuna kuiniliwa baada ya uaminifu,
Kama wewe sio mwaminifu unaiabisha imani uliyonayo wewe. Lakini pia uaminifu unathaminisha wokovu ulionao.

(C) Kuwa mwaminifu katika vyote ulivyo navyo(Mali na mapato yako)
Haswaa! hapa imetupasa kuwa waaminifu katika suala moja msingi kabisa ZAKA na sadaka..
Usiwemwizi wa zaka uwe makini usikose mbingu..

MUNGU ANATUPIMA UAMINIFU KWA YAPI?

- Nafasi tunayompa katika maisha yetu ya kawaida, tunamtambua Mungu kama nani?

- Pesa umeipa nafasi ya ngapi... Siku za mwisho watu watapenda pesa kuliko kumpenda Mungu. Wapo wanaochukiana kisa pesa..

-Biashara au shughuli inayokuingizia mapato, wengi wamekamatwa hapa, maana unaweza ukategwa kwa wateja kuongezeka muda wa ibada.

-Nadhiri na maagano.
Muhubiri 5:4 Ukimwekea Mungu nadhiri usikawie kuiondoa, Mungu hawi radhi na wapumbavu.
  Ni afadhali usiweke kabisa kuliko kuiweka na kutoitimiza.
-Muda wako kwa Mungu, je unampa Mungu nafasi, kuanzia wewe binafsi?. Unashiriki maombi na taratibu zote za ibada?   !!!!!Jitathmini!!!!
Luka 16:10
Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
He that is faithful in that which is least is faithful also in much: and he that is unjust in the least is unjust also in much.
Bila kuwa waaminifu haswa kwa mambo madogo kabisa hatuta mwona Mungu,
Nakazia tena sisi ni mabalozi wa Kristo hivyo imetupasa kuwa waaminifu sana mbele za Mungu na mbele za wanadamu.

Haijalishi ni tatizo ama uhitaji wa namna gani, sema kweli hata kama itakugharimu kwa sababu Uaminifu ni pamoja na ukweli.....
 
Usipende usingizi usije ukawa masikini, usingizi si hatar kwa maendeleo tu ya kiuchumi Bali hata kiroho, usiusikilize mwili ukaacha kuyatenda mapenzi ya Mungu..

Ukubwa au udogo wa jambo usikuchanganye!! Uaminifu ni katika mambo yote.

Mungu akubariki sana. Nakutakia wakati mwema.

Mwl. Faraja Komba

Monday, July 8, 2019

Hakuna mahusiano Bila Mawasiliano.

Na .Mwl Wetu..
Bwana Yesu asifiwe.
Developing Devotional relationship with God
Kuna aina saba za mahusiano
1: Wewe na Mungu
2: Wewe na mpenzi au mtu wa karibu sana mfano mke, mume au mchumba
3:Wewe na familia yako (mjomba n.k)
4: Familia hii na familia nyingine
5:Wewe  na Kanisa
6: Wewe na ufalme( wana wa Mungu ambao sio washirika wenzako katika kanisa moja)
7:Wewe na ulimwengu/dunia

Leo tutaangalia zaidi mahusiano kati yako na Mungu., haya yamebeba  msingi wa kila aina ya mahusiano unayopaswa kuwa nayo.

1. Uhusiano kati yako na Mungu  unaoneshwa na namna gani unamjua Mungu na kumpenda Mungu, Na kumjua Mungu nikulijua neno lake na kulitenda

Huwezi kusema unamahusiano na Mungu wakati huna mawasiliano naye.,Huenda mawasilano yenu yameingiliwa na jambo lingine..
   We have much time to pray but no time to listen from God.
Huwezi kuwasiliana na Mungu wakati wa uhitaji tu na ukasema unamahusiano mazuri na Mungu.
Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni lolote ..
 
Listening .. Unauwezo wa kumsikiliza Mungu?
Je unasoma neno lake??
Develop a Conversation with God

Relational prayer, kuna wakati unapaswa kwenda Mbele za Mungu kuimarisha uhusiano wako na Mungu na sio kwenda mbele zake kila saa for your needs/probpems

Reference
Mwanzo 3:24
Dhambi inadhoofisha uhusiano wako na Mungu.
Yohana 17:3
Mwanzo 3:8
 
Watu wengi wa Leo wanamuda mwingi wa social network kuliko muda wao na Mungu, hawawezi au wamesahau kutafuta relationship na watu kuliko Mungu.
Vijana wanatafuta wenzi wao kwa juhudi kubwa kuliko kumtafuta Mungu na kuimarisha uhusiano wao na Mungu.
  Make a room for God in your heart
...
Mungu akubariki tutaendelea wakati mwingine kwa neema ya Kristo. Nakusihi sana imarisha uhusiano wako na Mungu.
*Spend more time with God!!

Barrier/kikwazo kikubwa katika mawasiliano yetu na Mungu ni dhambi na uovu, 
Tukaze mwendo watumishi wa Mungu..
.... To be continued......

Mahali Casfeta Tayomi Mwecau. Monday Service.

Sunday, April 14, 2019

Heshimu ibada 2..

         *Mimi na ibada.*

  Muendelezo......
Kanuni ya Ki-Mungu ni kuomba kitu ndo upewe au kifanya kitu ndo ufanyiwe au ukirimiwe kwa kadri ya kunyenyekea/neema,... Hivyo usiende ibadani ukiwa unawaza uko mkamilifu Bali ukiwa na moyo wakuitaji jambo jipya tena na tena,. Moyo wa kushuka ulipondeka maana hao ndo watu Mungu anaowaangalia,.. Nenda na moyo wa toba (najua huna dhambi) lakini toba ni zaidi ya hapo.,
   Nenda ukiwa na shauku na mawazo yako yote kwamba utamuona Mungu Leo na hakika hatokuacha kama ulivyokuja.,
    Usiwe muheshimiwa mbele za Mungu tena wewe muheshimiwa ndo unyenyekee zaidi ,,
   Heshimu ibada.. *huwezi kumsababisha roho ashuke mbele za watu na afanye mambo mapya kama ukiwa mwenyewe hata hashuki, ukiwa mwenyewe hata uneni kwa lugha utawezaje sasa kusema unanena kwa lugha mbele za watu?*
   *Mungu wetu anasifa ya upya kila siku na habadiliki umewahi fikiri hili?*
     Taka jambo jipya kwa Bwana.
     Muheshimu Mungu kwa mavazi yako,. Acha mambo ya kuiga yasiyo tokana na Mungu, ama yaliyo na mashtaka na mashutumu.,(jitahidin kujionesha mmekubaliwa na Mungu)
     Nenda ibadani ukijua ya kuwa unaenda mbele za mfalme wa wafalme,. Kama unaweza kupendeza vizuri Fanya hivyo,. Ila uwe na kiasi sasa,. *Pia soma Walawi 10:10*
  David e k

Saturday, April 6, 2019

Heshimu ibada

*I believe 😊*  Ukianza kuona ibada sio muhimu sana kuliko masomo, kuliko kazi, biashara, n.k ujue kabisa unapaswa kufanya scanning ya iyo roho ngeni iliyokuingia kwa siri.     *#heshimu ibada, nenda ibadani, wahi ibadani, maanisha kuwepo ibadani, vaa kwa heshima ibadani, Fanya ulichokifuata ibadani, muabudu Mungu katika roho na kweli, usitoke kama ulivyoingia Bali utoke na badiliko kwa kupiga hatua zaidi kiroho, kiufahamu, kiafya, kiuchumi, ibada ni zaidi ya kitu muhimu kwako.* @davidek

Thursday, April 4, 2019

Kanuni ya Medali

*Haina maana kwamba wewe usipokua nafasi za juu kihuduma basi usimtafute Mungu, basi usiishi maisha matakatifu laa!!*
   *Nataka nikukumbushe kila kizazi kilikua na wacha Mungu wengi tu kumbuka wakati wa nabiii Yeremia hata manabii wa uongo walikuwepo, sasa unatoka wapi kusingizia msimu huu au kizazi hiki au teknolojia kua sababu ya wewe kutomcha Mungu?*    
     Kama wapo walioinuliwa zaidi yako kihuduma usiwachukie wapende nawewe jitahidi usiwaige ila upate na ufanye kile ambacho Mungu alikuumba ukifanye.
      *Pambana kila Siku hakikisha hakuna kikwazo kitakachokuzuia kufikia malengo na kusudi la Mungu katika maisha yako.*
     *🥇🥇🥇Mimi naiita hii kanuni ya medali,* *🥇🥇🥇  Wewe ni mshindi #1 ukifanya kwa juhudi, kwa malengo, bila kukata tamaa,.*
     
    Nakukumbusha pia unahitaji kujifunza nakuelewa wengine wanafanya nini na sababu za wao kufanya hivyo, lakini katika hili huitaji kujifunza kila kitu Mara moja hapana Bali kwa malengo zaidi na moja baada ya kingine
    *KILA SIKU NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU ITUMIE VIZURI*
   *Fanyia kazi kile kidogo unachofahamu, alafu ongeza uwezo kwa kuongeza ujuzi zaidi*
      *# usipoanza wewe wataanza wengine lakini kamwe hawatafanya kama ambavyo ungefanya wewe#*

   🔐David e kalebi.

Saturday, March 30, 2019

Viburi flow

      
Jipime kwa mawazo yako, nia ya moyo wako unapofanya jambo lolote ufanyalo, kusudio lako la ndani unapoamua kusema chochote unachosema na uhalisia wa muonekano wako unalenga nini? Jipime kama unauwezo wa kugeuka na kutubu,kama unaweza kusikiliza wengine kama unaweza kupokea maelekezo na kusikiliza hata kama unajua sana, jipime kama unaweza kuwapa wengine nafasi,? Je unajiona we we bora sana? Uko sahihi kama unaona wengine pia ni bora mno, *#Moyo wakunyenyekea
    Bwana Huwapinga wenye kiburi Bali huwapa wanyenyekevu neema.

GHARAMA YA USHINDI

  GHARAMA YA USHINDI 1. Utangulizi 2. Gharama ya ushindi 3. Kudumu kuwa mshindi Sehemu ya kwanza. Utangulizi   Kila jambo unalo ona limekwi...