*Mimi na ibada.*
Muendelezo......
Kanuni ya Ki-Mungu ni kuomba kitu ndo upewe au kifanya kitu ndo ufanyiwe au ukirimiwe kwa kadri ya kunyenyekea/neema,... Hivyo usiende ibadani ukiwa unawaza uko mkamilifu Bali ukiwa na moyo wakuitaji jambo jipya tena na tena,. Moyo wa kushuka ulipondeka maana hao ndo watu Mungu anaowaangalia,.. Nenda na moyo wa toba (najua huna dhambi) lakini toba ni zaidi ya hapo.,
Nenda ukiwa na shauku na mawazo yako yote kwamba utamuona Mungu Leo na hakika hatokuacha kama ulivyokuja.,
Usiwe muheshimiwa mbele za Mungu tena wewe muheshimiwa ndo unyenyekee zaidi ,,
Heshimu ibada.. *huwezi kumsababisha roho ashuke mbele za watu na afanye mambo mapya kama ukiwa mwenyewe hata hashuki, ukiwa mwenyewe hata uneni kwa lugha utawezaje sasa kusema unanena kwa lugha mbele za watu?*
*Mungu wetu anasifa ya upya kila siku na habadiliki umewahi fikiri hili?*
Taka jambo jipya kwa Bwana.
Muheshimu Mungu kwa mavazi yako,. Acha mambo ya kuiga yasiyo tokana na Mungu, ama yaliyo na mashtaka na mashutumu.,(jitahidin kujionesha mmekubaliwa na Mungu)
Nenda ibadani ukijua ya kuwa unaenda mbele za mfalme wa wafalme,. Kama unaweza kupendeza vizuri Fanya hivyo,. Ila uwe na kiasi sasa,. *Pia soma Walawi 10:10*
David e k